AliKiba akana kuandaa watu wamzomee Diamond Fiesta

Msanii anayefanya vizuri hivi sasa na wimbo wake wa Mwana 'Alikiba' amekanusha uvumi unaodai kuwa huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea Diamond Platnumz kwenye show ya Fiesta iliyofanyika October 18 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.


Alikiba amefunguka na kusema kuwa hajui uvumi huo umeanza vipi.

“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”

Mbali na hapo , Ali Kiba amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa ‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwahiyo waendelee kusubiri muda wowote.”
Previous Post Next Post