Fuse ODG Awashinda Davido, Wizkid Tuzo za Best Africa Act.#MOBO2014

Msanii kutoka Ghana anaye fanya vizuri Uingereza Fuse ODG na kwasasa ameamishia makazi yake hukohuko ameshinda tuzo ya Best African Act 2014 kwenye tuzo za MOBO za mwaka 2014. Hii ni mara ya pili kwa mfululizo Fuse anashinda tuzo hii. Fuse alikuwa akiwania tuzo hii na wasanii Davido, Wizkid, Mista Silva na Afrikan Boy.

Fuse ODG aka Nana Richard Abiona ameng’ara na nyimbo kama Antenna, Azonto na Million Pound Girl (Badder Than Bad). Wimbo wake mpya ‘Dangerous Love’ Ft Sean Paul ulifika namba mbili kwenye chati za Uingereza za nyimbo bora 40.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa