Penzi la Wiz Khlifa na Amber Rose laelekea ukingoni, chanzo kiko hapa

Penzi na Ndoa ya Wiz Khalifa na Amber Rose imefika ukingoni. Amber Rose anamshutumu Wiz Khalifa kuwa amekuwa akimsaliti kwa kipindi kirefu na kumtolea sababu zisizo na kichwa wala wa miguu.




Vyanzo vilivyo karibu na Amber, vimeiambia TMZ kuwa tangu kuanza kwa ziara ya Wiz, July mrembo huyo amekuwa akimhisi mume wake kuchepuka. Amber anawaambia marafiki zake kuwa alitaka kuungana na Wiz kwenye ziara hiyo lakini (Wiz) alikataa na kumtaka akae nyumbani kumwangalia mtoto wao.


Anadai kuwa Wiz anataka kumtawala zaidi kwa kusema yeye ndiye anatakiwa kutafuta mkate wa kila siku na Amber akae tu nyumbani.

Naye Wiz anadai kuwa ni Amber ndiye aliyemsaliti na Nick Cannon.





Kupitia talaka hiyo, Amber anataka kuchukua udhibiti wa mtoto wao Sebastian, mwenye umri wa mwaka mmoja lakini atamruhusu Wiz kumtembelea mwanae. TMZ imedai imeziona nyaraka za talaka ambazo zinaonesha kuwa wapenzi hao waliachana Jumatatu hii kwa kile kilichodaiwa tofauti zisizosuluhishika.

Previous Post Next Post