Audio: Hivi ndivyo wimbo wa mwana FA na G Nako wa Mfaleme uivyofanyika

Mwana FA amerudi kwa kasi kwenye headline wiki hii baada ya kuachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Mweusi, G-Nako uitwao ‘Mfalme’ na ambao aliutambulisha kwa kuutumbuiza live kwenye tuzo za Kilimanjaro Jumamosi iliyopita.



Amesema aliuandika wimbo huo baada ya kupata mawazo kuwa kuna wakati inatakiwa kuacha kulalamika na kuamua kumshukuru tu Mungu kwakuwa kuna watu wenye matatizo zaidi. Ameongeza kuwa wazo la wimbo huo lilikomaa zaidi baada ya kutumiwa beats sita na Nahreel na yeye kuichagua hiyo peke yake.

“Niliipenda kwasababu ilikuwa na sample za kimasai nikafikiri ni kitu ambacho unaweza kukifanya kikubwa sababu always unajua matatizo yanayotukabili ni kwamba muziki wetu kutoka ni kwasababu tunataka kushindana na watu wengine ambao wanafanya muziki huo huo wakati tunaweza kuingiza muziki wetu tukafuse some of our music ambao tunataka uende kimataifa ukaeleweka kirahisi zaidi,” amesema.

Mwana FA amesema pamoja na kuimba chorus, G-Nako ana mchango mkubwa kwenye wimbo huo.

“Actually kazi aliyoifanya G-Nako ndio imenyoosha kila kitu. Idea yangu niliyokuwa nayo ilikuwa tofauti kabisa. Nimeenda studio, G-Nako alivyofanya chorus i had to take beat na chorus sasa niende nikaandike upya. Verse ya kwanza nilikuwa na verse nyingine nilirekodi nikaiondoa, nikaweka verse nyingine nikaiondoa, hii ambayo unaisikia ipo humo ni ya tatu.”

“Unajua FA ni msanii mkali, G-Nako ni msanii mkali kwahiyo mara nyingi collabo kama hizi zikitokea na feeling yenyewe ikawepo zikifanyika always zinakuwaga kitu kikubwa,”

“FA aliponipa jukumu kama lile, nililitekeleza kama inavyotakiwa.”

Previous Post Next Post

Popular Items