| Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),akifafanua jambo katika mkutano wa kujadili namna bora ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani,Kulia kwa Mkurugenzi wa SUMATRA ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.Kulia kwa Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe.Pereira AmeSilima (aliyevaa suti nyeusi)ni Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe na kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi(Mb). Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi,Said Mwema akichangia jambo katika Mkutano uliowakutanisha Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe(Mb) aliyevaa suti nyeusi,na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi(Mb) aliyevaa suti ya kaki.Mkutano huo ulifanyika Wizara ya Uchukuzi na kuwakutanisha SUMATRA,Jeshi la Polisi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na viongozi mbali mbali wa Wizara ya Uchukuzi lengo likiwa kujadili namna ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani Nchini |