Master J kufunguka hadharani kuhusu Shaa karibuni

Mtayarishaji muziki Master J, ambaye siku ya jana kupitia Kikaangoni Live ya Facebook EATV, amekiri hadharani kuhusiana na mahusiano yake na msanii Sarah Kaisi maarufu kama Shaa, ameiambia eNewz kuhusiana na mpango wa kuweka mambo hadharani rasmi.


Master J amesema, katika siku za karibuni ataitisha mkutano na waandishi na kuweka wazi rasmi kuhusiana na kinachoendelea kati yake na Shaa na kutangaza mipango yao ya baadaye.

Master J amesema kuwa, amekuwa akikutana na maswali mengi kuhusiana na yeye na Shaa na hata mama yake mzazi amemshauri kuwa, kuna haja ya yeye kuliweka suala hili wazi, na hii ikiwa ni mara ya kwanza na rasmi kabisa kwa Master J kuzungumza kuhusiana na yeye na Shaa.

Akiwa katika hali ya kutabasamu na kutotaka kutoa uhakika wa moja kwa moja, Master J amesema kuwa, swala la ndoa kati yake na Shaa litawekwa wazi kwa watu wote ukifika wakati ambapo ataona kuwa inafaa kufanya hivyo.

Previous Post Next Post