TANZANIA YATAKA MALENGO MAPYA YA MAENDELEO ENDELEVU YATOE KIPAUMBELE KUPUNGUZA UMASKINI



Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akifuatilia kwa makini majadiliano ya Mkutano wa pili uliokuwa ukijadili uandaaji wa malengo mpya ya maendeleo endelevu ( SDGs).
Mkutano huo ulifanyika kwa siku tatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na ni mmoja wa milolongo ya mikutano ya majadiliano yanayolenga kuunda malengo hayo endelevu ili kuendeleza maudhui ya malengo ya Milenia ambayo mipango yake itafikia tamati Mwaka 2015.


Tanzania ni kati ya nchi Thelathini ambazo zimechaguliwa kuongoza majadiliano hayo. Akichangia majadiliano hayo, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na mambo mengine alisisitiza kwamba malengo mapya ya maendeleo pamoja na kuzingatia mihimili mitatu ya ajenda za maendeleo yaani uchumi, jamii na mazingiria, suala la kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini lazima liwe lengo kuu katika malengo hayo mapya.Nyuma ya Balozi, Ni Afisa Ubalozi Mwandamizi, Bw. Modest Mero
Previous Post Next Post

Popular Items