Audio: Country Boy asimulia alivyopewa kesi ya kujaribu kumbaka mwanafunzi..

Kweli sio kila anaekwenda jela ana hatia na kwamba wengine wamekwenda kwa kesi za kusingiziwa.

Hii ingeweza kumkuta rapper wa kundi la Mtu Chee, Country Boy ambaye anadai aliwahi kusingiziwa kufanya jaribio la kumbaka msichana wa sekondari wakati yeye pia akiwa kidato cha nne.

Rapper huyo amesimulia tukio hilo kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm, ambapo anatoa simulizi la maisha yake na muziki akiwa kama mkali wa The Jump Off wa wiki hii.


Country Boy anaeleza kuwa walikuwa kwenye party ya shule ambayo ilikuwa imefanyika kuikaribisha wiki ya mitihani. Na kwamba kwenye party hiyo kulianzishwa mashindano ya kurap ambayo yaliwahusisha wavulana wa kidato cha tatu na cha nne.

Ameeleza kuwa yeye aliwakilishwa na rafiki yake ambaye kwa bahati mbaya alikuwa hajui kurap hivyo akazomewa sana, lakini kwa mara ya kwanza Country akaamua kurudisha heshima ya rafiki yake kwa kupiga freestyle iliyopelekea umati kumkubali na kumshangilia. Wasichana nao walikuwa msitari wa mbele kushow love kwake kitu kilichowafanya washikaji zao kumbambikizia kesi ili kumzima.

“Wale wana kiskul skul madem zao wakawa wote wananikubali mimi. Sasa wana wakanitengenezea msala nini, nikakutana nao mbele ugomvi wa maana. Kesho yake nikapewa kesi kuwa eti msichana wa watu nilikuwa nataka nikambake. Ndo hivyo ikawa kesi kubwa mpaka bibi mkubwa ilimshitua yaani kinoma noma.” Amesimulia Country Boy.

Mpango wa wavulana hao na ushahidi wa uongo uliotolewa na msichana huyo ulimsababishia adhabu kali Country Boy ili afanye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.

“Yaani hiyo siwezi kuisahau kwa sababu nilipigwa fimbo 58 ili nisamehewe nikafanye mtihani.” Ameeleza.

Hata hivyo, Country aliitumikia adhabu yake na baada ya kumaliza shule na kuwa mtaani na kufanikiwa kuwa rapper mdogo mwenye jina kubwa, alikutana na msichana huyo aliyemsingizia kesi ile, na hapo akiwa amekuja kuangalia show yake club.

“Nilikutana nae club nilikuwa na show, nikamuangalia tu. Sikuweza kufanya chochote kwa sababu nakumbuka yalikuwa mambo ya kiskul, ananikumbuka…sikupata nafasi (ya kuongea nae) kwa sababu alikuwa na kampani yake halafu wanaume na nini. Siwezi kujua kama tabia yake imebadilika au hajabadilika yanaweza yakawa kama yaleyale tena, si unajua wabongo.” Ameeleza.

Country Boy ameleza kuwa ameshamsamehe msichana huyo japo ni tukio ambalo hatalisahau.

Msikilize hapa..!


Source:Timesfm!
Previous Post Next Post