Sababu za Dully Sykes kuahirisha kutoa wimbo aliofanya na Diamond 'Chipolopolo' na kutoa Togola,

Dully Sykes ameahirisha mpango wa kuachia rasmi wimbo aliofanya na swahiba wake Diamond Platinumz alioupa jina la Chipolopolo na badala yake ataachia wimbo alioupa jina la ‘Togola’ mwezi huu.

Mkali huyo wa Shikide, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa ameamua kufanya mabadiliko hayo kutokana na muziki unavyobadilika.



“Kutokana na muziki kubadilika, unajua mimi nafanya muziki kutokana na jinsi unavyobadilika. Jinsi muziki unavyobadilika imebidi nifanye hivyo. Ni uchaguzi tu wa nyimbo kwa sababu nina nyimbo nyingi kwa hiyo sioni sababu za kung’ang’ania wimbo mmoja wakati nina nyimbo nyingi.”

Hata hivyo, mkali huyo amesema Chipolopolo ipo na anaeitaka atampatia na kwamba tayari wimbo huo upo kwenye miito ya simu. Ameongeza kuwa wataufanyia video baadae lakini sio kwamba utakuwa umetoka officially.

Akiongelea kuhusu maana ya Togola, Dully amesema hata yeye hafahamu maana yake na ni neno limekuja tu kama ilivyokuwa ‘Shikide’ lakini ameambiwa kuwa Tanga neno Togola ni salamu.
Previous Post Next Post