HIKI NDICHO KILICHOMPELEKA RAY DUBAI! AONGEZA NGUVU MPYA KATIKA KAMPUNI



Kilichompeleka
Baada ya kupotea nchini kwa takribani wiki mbili hatimaye mwigizaji mwenye mafanikio makubwa sana nchini Vicent Kigosi “ Ray” Amerejea Tanzania Tokea Dubai na vifaa vipya kabisa na vya kisasa kwa ajili ya utengenezaji wa filamu chini ya kampuni yake ya RJ company yenye makao makuu huko sinza Dar es Salaam.
Ray ambaye aliondoka nchini takribani wiki nne zilizopita amekuja na vifaa ambavyo ye mwenyewe anasema hamna mtu wala mwigizaji yoyote anayetumia vifaa kama hivyo Afrika mashariki na kati kwa ajili ya filamu.
“Unajua soko la filamu linakua, kila siku teknolojia inaongezeka na kuwa kubwa, tukiendelea kulala na kutumia vifaa vyetu vya kizamani hatufiki popote, ndo maana nimeamua kuja na vitu ambavyo naamini vitaobgeza ubora wa filamu zetu” 


              Picha ya baadhi ya vifaa alivyoenda kuongeza Ray nchini Dubai




Previous Post Next Post