Lulu ajipanga zaidi katika soko la Bongo Movie baada ya kutoka jela..arejea na mbinu hizi.

Mwigizaji maarurfu wa bongomovies Elizabeth Michael ama Lulu, bado hajawa teyari kwa ajili ya kuzungumza na vyombo vya habari vingi vinavyotafuta kufanya naye interview baada ya mrembo huyu kuachiliwa kwa dhamana kuhusu kesi inayomkabili kuhusiana na kifo cha marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake.



Taarifa za kuaminika zilizopatikana toka kwa mmoja wa watu wa karibu sana na Lulu zinasema kuwa, mwanadada huyu atakuwa huru kuzungumza na vyombo vya habari katika siku chache zijazo ila kwa sasa kwani bado anapata mapumziko ya binafsi na pia anajiandaa kutoka na filamu mpya ambayo ndiyo itakuwa kama utambulisho mpya wa mwigizaji Elizabeth Michael baada ya kutoka jela alipokuwa akishikiliwa kwa takribani mwaka mmoja.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA