RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MUUNGANO UWANJA WA UHURU LEO










Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali ili kushuhudia maadhimisho hayo.Rais Dk. Jakaya Kikwete akikagua kikosi cha Jeshi la Magereza wanawake wakati wa maadhimisho hayo


Rais Dk. Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayoRais Dk. Jakaya Kikwete akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine kutoka kulia ni Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.


Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kulia akiwa na viongozi wengine katika jukwaa kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiingia uwanjani katika gari maalum huku akisindikizwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Uhuru


Msafara wa Rais ukiingia uwanjani leo


Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ kikipita na kutoa heshima mbele .


Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ wanamaji kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete .


Kikosi cha Jeshi la Kujenga taifa JKT kikitoa heshima mbelea ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.



Kikosi Maalum Cha Bendera kikitoa heshima zake bele ya Rais Jakaya Kikwete


Kikosi chamJeshi la Ulinzi JWTZ nchi kavu kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.


Kikso cha Askari wa Magereza kikipita na kutoa heshima mbele ya Rais Jakaya Kikwete


Watoto wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika maadhimisho hayo



Watoto wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika maadhimisho hayo
Previous Post Next Post