Gardner: Nimesota, nimetoka

Mtangazaji maarufu wa redio nchini anayeendesha kipindi cha Maskani katika kituo cha Times FM, Gardner Habash ameweka wazi kuwa umaarufu wake haukuja kirahisi. Gardner alisema mafanikio aliyokuwa nayo yametokana na uvumilivu.


Alisema kabla ya kuanza kuvuma katika redio alikuwa kibarua katika kiwanda cha bia jijini Mwanza akifanya kazi ya kupakia na kupakua kreti za bia.

“Nawaomba vijana wasichague kazi. Binafsi nilikuwa nabeba kreti za bia katika kiwanda Mwanza kabla sijapata wasaa wa kufanya mambo mengine hadi kufikia utangazaji,” alisema Gardner.

Kaa tayari kupata makala zaidi kuhusu maisha yake na misukosuko ya ndoa na mwanamuziki Lady Jay Dee.
Previous Post Next Post

Popular Items