Lameck Kanumba, ambaye ni mdogo wa aliyekuwa mwigizaji nyota nchini marehemu Steven Kanumba, anatarajia kuachia filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘Asante Mama’
Alisema huo ni ujio wake mpya katika kuendeleza kile kilichokuwa kikifanywa na kaka yake enzi za uhai wake. Lameck alisema amepata nafasi ya kushiriki filamu hiyo iliyoandaliwa na baadhi ya wasanii waliokuwa wakifanya kazi pamoja na marehemu Kanumba, Mayasa Mrisho na Ben Branko (Serengo).
Aliongeza kuwa ana filamu hiyo imani itafanya vizuri sokoni na hivyo kuwa katika mstari mzuri wa kusonga mbele katika tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Tags:
From Bongo Movies