Picha: Ajali nyingine mbaya ya basi la abiria yasababisha vifo maeneo ya Gairo

Basi la abiria linalomilikiwa na kampuni ya Airbus linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tabora limepata ajali mbaya leo mchana katika eneo la Kiegeya, Gairo na watu wanne wanahofia kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.


Sababu za ajli hiyo hazikufahamika haraka lakini mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza kuwa maafisa wa usalama walifika mapema katika eneo hilo na shughuli za uokoaji zilifanyika mapema.


Ajali hiyo ni mwiba mwingine mkubwa kwenye mioyo ya watanzania wenye majonzi ikiwa ni siku mbili baada ya kutokea ajali mbaya iliyochukua uhai wa zaidi ya watu 40 katika eneo la Kiabakari, Musoma, Mara.
Previous Post Next Post