P-Square wamshirikisha Awilo Longomba kwenye hii album yao mpya itakayotoka Sept 12

Hivi karibuni P-Square wali’share’ picha wakiwa na mkongwe kutoka DRC mwimbaji wa ‘Bundelele,’ Awilo Longomba ambaye alikuwa Nigeria, na kuandika kuwa kuna kitu kikubwa kinakuja, “Will let y’all knw what we are celebrating soon….Just wait for It. Cos it’s a big one! #P-Classic.”




Inawezekana tayari fumbo hilo limefumbuliwa baada ya kundi hilo kutoa cover ya album yao mpya ‘Double Trouble’, ambayo inatarajiwa kutoka September 12. Katika orodha ya nyimbo 13 zitakazopatikana kwenye album hiyo ya sita kwa kundi hilo, wimbo namba 10 uitwao ‘Enemy Solo’ wamefanya collabo na Awilo Longomba.




Album hiyo pia itakuwa na bonus ya nyimbo zao tatu ambazo zimeishatoka. Wengine walioshirikishwa T.I, Dave Scott, Jermaine Jackson na Don Jazzy.

Previous Post Next Post