Britney Spears amchimba mkwara mzito mwanamke aliyechepuka na mpenzi wake

Britney Spears ameamua kuweka siri nzito yote yaliyotokea kati yake na mpenzi wake wa zamani David Lucado aliyechepuka na mwanamke aliyetajwa kuwa ni star wa filamu za ngono, Cali Lee.



Kwa mujibu wa TMZ, timu ya Britney Spears imemtumia Cali Lee ujumbe wa vitisho wakimuonya asifungue mdomo wake kueleza chochote walichoongea na David Lucado kuhusu Britney Spears wakati wanachepuka.

Katika hatua nyingine, watu wa timu ya Britney wameiambia TMZ kuwa Lucado na mwimbaji huyo wamesaini makubaliano maalum kisheria ya usiri kuhusu mapenzi yao na Lee pia amebanwa.

Hata hivyo, mwanasheria wa Lee amesema kuwa mteja wake habanwi kabisa na makubaliano hayo na kwamba yuko huru kuzungumza chochote kinachomhusu.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA