Alichoamua Britney Spears baada ya kuona video ya mpenzi wake akimsaliti

Mwimbaji Britney Spears amevunjwa moyo baada ya kushuhudia kipande cha video kilichovujishwa kikimuonesha mpenzi wake David Lucado akimsaliti na msichana ambaye hakutambulika kwa haraka.



Katika video hiyo, David Lucado anaonekana akicheza na msichana huyo huku akimkiss kama wanaigiza filamu ya mahaba na wao ndio wahusika wakuu.

Britney Spears ameshindwa kuvumilia alichokiona na ameamua kumpiga chini Lucado na hivi ni single girl.


“Aahhhh! The Single life.” Ametweet Britney.

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya E! Entertainment, Lucado anaamini bado kuna nafasi ya kuongea na kurudiana na mwimbaji huyo.

Ripoti nyingine zimeeleza kuwa Britney Spears ameanza kuwasiliana na boyfriend wake wa zamani Adnan Ghalib.


Previous Post Next Post

Popular Items