Picha: Pastor Myamba azungumzia bajeti ya harusi yake na maisha mapya baada ya kuoa

Msanii mkongwe wa filamu nchini Emmanuel Myamba, amezungumzia bajeti ya harusi yake iliyodaiwa ilikuwa ya kifahari pamoja na maisha yake mapya baada ya kufunga ndoa.


Pastor Myamba akiwa na mke wake Praxceda

Myamba ambae amefunga ndoa na mwanadada Praxceda huko visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwezi August,

“Namshuru mungu ndoa ilipita salama kama ulivyosikia, unajua budget ya ndoa sikufufichi ilikuwa kubwa ila kusema kwamba ni shilling fulani nitakudanganya, kamati ndo ilikuwa inajua kila kitu ila ndoa ilikuwa kubwa sana, dah kusema kwamba ndoa ilikuwa ya milioni 100 au pungufu nitakuwa sikutendei haki kwa sababu budget sijui ilikuwa kubwa kiasi gani, nawashukuru sana wasanii wengangu ,ndugu, jamaa na marafiki waliyowezesha harusi ikawa kubwa, pia kuna dada yangu ambaye alinizawadia gari na vitu vingine” Alisema Myamba.

Pia Myamba amesema baada ya kuachana na ukapela kuna mambo mengi yamebadilika katika maisha yake.

“Baada ya kuoa najiona mwepesi, unajua maisha ya ubachela yana tabu zake ila sasa hivi nipo safi maisha naona mazuri, kazi zinaenda vizuri, sijawai kuwa na mtoto nazani sasa hivi ndiyo muda muafaka mungu akipenda” Alimalizia Myamba.








Credit:Bongo5
Previous Post Next Post

Popular Items