Baada ya kuandikwa na Gazeti la Udaku kuwa na mahusiano na 'dogo dogo' Lady Jaydee ajibu habari hiyo

Mwanadada Lady Jaydee ameamua kujibu habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku la Risasi kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’.



Kwenye habari hiyo, Risasi wanadai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.



Kupitia Instagram, Jaydee ameandika:

Kuna habari za kuniudhi Ila hii imenichekesha. Kwahiyo mtoto wa vitoto ndio bwana angu???? Basi sawa nashukuru naona mmenianzia tena sasa picha za February Na nilizi post mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona? Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua ,,, wangapi wameshapiga picha na hiyo Range? Duuuh! !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma. Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo hapa hapa.”
Previous Post Next Post

Popular Items

HOW TO LOOSE GOOD WOMAN

5 THINGS YOU DON'T KNOW ABOUT LIL COOL J