Ommy Dimpoz kuwashirikisha Yamoto Band kwenye wimbo wake mpya

Ommy Dimpoz amepanga kuwashirikisha vijana wanne wa Yamoto Band kwenye wimbo wake mpya.



Ommy amedai kuwa vijana hao wanafanya vizuri kwa sasa na angependa kuleta ladha mpya kwenye wimbo wake. “Vijana wana vipaji na ni wakali, nimebahatika kusikiliza nyimbo walizotoa na ambazo hazijatoka kwahiyo nafikiri ni kitu kizuri kufanya nao kolabo,” amesema Ommy.

Amesema wimbo huo wataurekodi kwenye studio za Combination Sounds na akiwa ni mtayarishaji Man Walter, mshindi wa tuzo za KTMA 2014 kama mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya.



Hata hivyo Ommy amedai kuwa wimbo huo aliutunga tangu akiwa na Top Band japo hakuwa amepata watu muafaka wa kuwashirikisha.
Previous Post Next Post