AY na Diamond kulipia video ya wimbo wa Chidi Benz ‘Mpaka Kuchee’

AY na Diamond Platnumz wamedhamiria kumrejesha tena kwenye chart rapper Chidi Benz ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu. Wasanii hao waliofanikiwa zaidi, wameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Chidi uitwao ‘ Mpaka Kuchee’ uliotayarishwa na Dully Sykes.



Pamoja na kugharamia utengezaji wa wimbo huo, AY na Diamond watagharamia pia utengezaji wa video yake ambao utaanza hivi karibuni. AY amedai kuwa watahakikisha wanausimamia wimbo huo hadi ufanikiwe kwakuwa Chidi ni msanii mwenye kipaji ambaye pamoja na matatizo yake binafsi, wasingependa kuona kinapotea.

Chidi ametoa shukrani kwa wasanii hao kwa jinsi walivyojitolea kumsaidia. “Mpaka kucheeeee… Thanks kwa uwezo. Thanks kwa Dimoond, Ay bajajeee, Dully Sykes na wengine wengine. Aisiii,” alitweet Jumamosi hii.

Chidi Benz amekuwa kwenye misukosuko mingi katika miaka ya hivi karibuni na aliwahi kukiri kujaribu kuacha matumizi ya dawa za kulevya. “Tunapitia vingi na vyote ni Mungu amepanga na ameandika, ninaamini hivyo kwa imani yangu najaribu kukukaribisha na wewe pia. Tufanye kazi,” aliandika rapper huyo kwenye Twitter.
Previous Post Next Post