Mwana FA , AY, Victoria Kimani, D’Banj, Yaya Toure na wengine Kihudhuria White House, Marekani

AY na Mwana FA wataungana wasanii wengine wakubwa barani Afrika wiki ijayo nchini Marekani, kwa mwaliko kutoka ikulu ya Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika utakaofanyika wiki ijayo.




Wasanii hao ni sehemu ya wale walioshiriki kwenye mradi wa One Campaign. Wasanii wengine waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Femi Kuti, Owamumi na D’Banj wa Nigeria, wa Afrika Kusini na Fally Ipupa wa DRC, Victoria Kimani wa Kenya, watakaoungana na mchezaji Manchester City, Yaya Toure mjini Washington D.C. kuanzia August 4-7.

Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka barani Afrika kwenye mji huo mkuu wa Marekani katika mkutano wa siku tatu. Huo ni mkutano mkubwa zaidi kuwahi kufanyika kati ya Rais wa Marekani na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali za Afrika.

Kwenye ziara hiyo, wasanii hao watakutana na viongozi wa juu wa serikali Marekani, wajumbe wa taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) na wajumbe wa Congress. Pia watatumbuiza siku ya August 4 ukiwemo wimbo wao wa ‘Cocoa Na Chocolate’.
Previous Post Next Post