Professor Jay atoa Darasa huru kwa wasanii kuhusu Mameneja wa 'Kibongo'

Mfumo wa menejimenti za wasanii Tanzania umekuwa kilio cha muda mrefu kwa pande zote mbili, wasanii wakiwalalamikia wale wanaowaita mameneja huku mameneja hao kwa namna moja au nyingine.

Kufuatia mijadala hiyo, rapper mkongwe, Profesa Jay ametoa ushauri wake kwa wasanii wa Tanzania Profesa Jay Ameshauri wasanii kutokubali kuwa chini ya mameneja ambao hawana taaluma hiyo, wanaovaa jina la umeneja kwa kigezo cha kuwa na pesa ya kuwasaidia wasanii.



“Unajua wasanii wa Bongo wengi tumekuwa hatutaki kufanya shughuli hizi wenyewe. So wengi wanakimbia kwa watu wenye senti zao lakini hawana hata idea ya muziki wanakuwa wanahodhi wasanii. Matokeo yake sasa badala ya kuelekea China mnakuwa mnaelekea Gongo la Mboto. Kwa sababu anaekumeneji na kufanya vitu vingine, ana hela tu yuko nyumbani.” Amesema Profesa Jay.

Rapper huyo ambaye ameachia wimbo mpya ‘Tatu Chafu’, ameeleza kuwa meneja ni mtu ambaye anatakiwa kuwa mpiganaji anaemtafutia msanii njia za kutoka na kufanya shows nyingi kadiri iwezekanavyo na kwamba wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakipenda vitu vya short-cut na ndio sababu wanafikia hatua ya kuangukia mikononi mwa watu wenye pesa wasio na taaluma ya umeneja.

“Hawezi kulala meneja kuanza kusubiri eti hadi simu ilie ‘ebana namhitaji Profesa Jay huku Kahama’, huyo sio Meneja. Sio meneja huyo, meneja anaangalia masoko ya Profesa Jay, wapi muziki wake utafika, wapi anaweza kushirikiana na nani ikafika na vitu kama hivyo.

“So, hayo makundi yapo, ni watu wenye hela zao. Kwa sababu ya uvivu wa wasanii kutoinvest kwenye muziki na kutaka shortcut. Unaona daah! Yule mchini ana hela ngoja niende tu’. Unamfuata unasema ‘braza eeh mimi naweza kuimba..braza nisaidie’. Sasa huwezi kujua huyo jamaa anauza matunda, anauza nini lakini anasent zake tu inabidi akumeneji. Matokeo yake unakuta wewe na yeye wote mnapotea.” Amefafanua Profesa Jay.

Amesema hiyo ni sababu iliyomfanya yeye ashindwe kuwa na meneja na badala yake kuwa na washikaji ambao wanaweza kumsaidia kama marafiki badala ya kuwa na meneja ambaye anachofanya ni kulipia gharama za audio na video tu.

“Ndio maana wasanii tunakuwa wengi lakini wanaotaka kufanya muziki kwa dhati wanakuwa wachache. Sasa inafika town inabidi tukubaliane na tuchuje. Sasa hawa ndio wasanii wa kuzunguka hapa hapa downtown tuwaache hapa hapa downtown na wale tunaotaka kwenda international twende tu hata kwa lazima…”
Previous Post Next Post