Tyga aitosa ziara ya Wiz Khalifa

Rapper Tyga aliyekuwa anategemewa kumsindikiza Wiz Khalifa kwenye ziara yake ya ‘Under The Influence Of Music’ ametangaza kuitosa ziara hiyo kupitia Twitter.

Alhamisi, July 10, Wiz Khalifa aliwataarifu mashabiki wake uamuzi wa Tyga na kuwaomba radhi kwa maneno mafupi.




“Tyga dropped off the tour. Sorry ya’ll.” Wiz Khalifa alitweet.

Nae Tyga alitoa sababu za uamuzi wake baada ya Wiz kotoa taarifa hiyo ambapo amedai atakuwa busy akishughulikia albam yake mpya na filamu yake.

“Nilitaka kuwa sehemu ya ziara. Lakini nimemaliza. Nashughulikia albam yangu na nashuti filamu.” Inaeleza tweet ya Tyga.

Tyga yuko katika pilikapilika za kuhakikisha albam yake ‘The Gold Album: 18th Dynasty’ inakuwa albam kubwa itakayotoka baadae mwaka huu.
Previous Post Next Post