Wema azungumzia video mpya za Diamond, na Jinsi Diamond alivyomkutanisha na waigizaji wa kimataifa

Diamond Platinumz alipokewa kwa shangwe jana (July 10) katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere na wadau mbalimbali wa muziki na mashabiki wake akitokea Marekani alikoenda kushiriki katika tuzo za BET.

Wema Abraham Sepetu alifika pia katika uwanja huo kumpokea asali wake wa Moyo na alipata nafasi ya kuzungumza na Fadhili Haule, mtangazaji wa kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm aliyetaka kupata maoni yake kuhusu video mbili mpya za Diamond zilizotoka hivi karibuni ‘MdogoMdogo na Bum Bum aliyomshirikisha Iyanya’.



Wema alifunguka huku akiweka akilini kuwa anamzungumzia asali wake wa moyo hivyo lugha na points zote alizitumia vyema.

“Well, honestly nimeipokea vizuri. Kitu chochote anachokifanya mpenzi lazima utakiona kizuri hata kama ni kafanya kibaya utakiona kizuri tu. Kwa hiyo amejitahidi, he is on another level na huwezi kumfananisha na msanii yoyote Tanzania na haangushi mashabiki wake. Unachokitegemea anafanya zaidi” Amesema.

Ameeleza kuwa kwenye video ya MdogoMdogo alifanya kitu tofauti na watu walichokuwa wanategea kwa jinsi wanavyomfahamu Diamond na mitindo yake.

“Watu walikuwa wanategemea kuwa video itakuwa…labda ataenda uswahilini sijui nini, lakini yeye kaifanya very international and nimeipenda the fact kwamba kuna uinternational lakini pia kuna uafrika ndani yake, so it’s nice.”

“Bum Bum, it’s nice. Like Bum Bum imeenda sana International like soko la nje sanasana. Na ndio maana hamjaona akirelease audio yake. And the video…yaani everything is nice, siwezi kum-criticize baby wangu.” Ameeleza Wema Sepetu.

Katika hatua nyingine, Wema ambaye ameahidi kuwa pamoja na Diamond katika yote amesema tayari ameshazungumza nae kuhusu hatua aliyoifanya ya kumkutanisha na waigizaji wa kimataifa na mashabiki wao wakae mkao wa kupokea kitu kikubwa katika tasnia ya filamu.

Kipindi cha Sunrise kinakuwa hewani kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili asubuhi.
Previous Post Next Post

Popular Items