Linah azungumzia collabo &Video alizofanya Afrika Kusini na mkataba mnono aliosaini

Sanaa ya muziki wa kizazi kipya Tanzania inazidi kukomaa mabawa na kuruka vyema kwenye level za kimataifa. Ndege Mnana aka Linah amejiunga na orodha ya wasanii wa kike wa Tanzania kama Lady Jay Dee ambao wameshafanya collabo na wasanii wa kimataifa kwa kutumia nafasi aliyoipata akiwa Afrika Kusini.

Akiongea na Times Fm, Linah ameeleza mafanikio aliyoyapata kwenye safari yake hiyo iliyomchukua takribani mwezi mzima, amefanya nyimbo na wasanii wakubwa wa kundi la Uhuru la Oskido, Mr Flavor na wengine wengi.




“Cha kwanza kabisa nimefanya na Uhuru. Uhuru ujue ni kundi ambalo liko chini ya Oskido. Kampuni yake inaitwa Kalawa, kwa hiyo Kalawa imewasainisha hao Uhuru. Wana producer wao ambaye ameproduce hit songs nyingi sana za Afrika kwa ujumla. Nimefanya kazi pia na huyu DJ anaeitwa Malvado kutoka Angola ambaye pia nimefanya nae.”

Akielezea kuhusu jinsi alivyopata nafasi ya kufanya kazi na DJ huyu maarufu, amesema kuwa alipigiwa simu saa nane usiku na producer wa kundi la Uhuru ambaye alimtaka aende studio kufanya kazi na alimueleza kuwa nafasi hiyo imepatikana baada ya DJ Malvado kusikiliza baadhi ya nyimbo za Linah alizorekodi katika studio hiyo.

Mwimbaji huyo pia amefafanua pia kuhusu umiliki wa nyimbo alizofanya.

“Wimbo wangu ambao nimefanya nimemshirikisha jamaa wa Uhuru ambaye anaitwa Xele, na vilevile ndio nimefanya collabo na huyo Malvado. Vilevile Mr Flavor, ambapo Mr Flavor kuna wimbo ambao mimi nilifanya akaingiza sauti ila hakupenda kwa hiyo akasema nikirudi nitarudia tena sauti. Wimbo ni wa kwangu.”

Linah amepanga kurudi Afrika Kusini hivi karibuni kufanya video na kampuni ya GodFather ambayo imetuma audio ya wimbo wake kwa baadhi ya vituo vikubwa vya runinga vya kimataifa ambavyo vimeikubali na hivyo vinasubiri video nzuri maisha yaendelee.

Sio hayo tu, msanii huyo amemwaga wino kwenye kampuni ya matangazo ya huko kwa Madiba.

“Nimesaini Contract na kampuni kubwa ambayo iko South Africa, before walikuwa wanadeal na masuala ya matangazo lakini sasa hivi kampuni imekuwa kubwa na wanataka kufanya kazi na wasanii kama label. Na mimi ni msanii wa kwanza kwao kwa sababu kuna baadhi ya wafanyakazi wa hiyo kampuni ni watanzania….”

Usikose kusikiliza Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kesho (Jumamosi) kuanzia saa kumi kamili hadi saa moja kamili utamsikia Linaha akielezea kiundani.
Previous Post Next Post