Maelezo ya wakili wa Emmanuel Mbasha yaleta utata, kesi yaahirishwa hadi July 23

Emanuel Mbasha ambaye ni Mwimbaji wa injili, amepandishwa tena kizimbani leo, July 17 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka mawili yanayomkabili katika kesi ya ubakaji.

Akiwa mahakamani hapo, Mbasha aliiomba mahakama kuahirisha kwa muda wa nusu saa kesi hiyo ili kumpa nafasi wakili wake kufika mahakamani hapo kwa madai kuwa alicheleweshwa na foleni.

“Unawakili? Au unatangaza nia ya kuweka wakili” Aliuliza hakimu Luago anaesikiliza kesi hiyo. Aliuliza Hakimu Wilbert Luago anaesikiliza kesi hiyo.


Emmanuel Mbasha akiwa Mahakamani

Hata hivyo, mheshimiwa hakimu alilikubali ombi la Mbasha na kuahirisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa mujibu wa sheria.

Baada ya kurejea, wakili aliyemuwakilisha wakili huyo wa Mbasha aliwasilisha barua ya dharura inayoonesha kuwa yuko jijini Arusha akihudhuria kesi nyingine, maelezo yaliyokuwa tofauti na maelezo ya awali.

Hata hivyo, hakimu alilikubali ombi hilo nakuahirisha kesi hiyo hadi July 23, mwaka huu huku akimtaka Mbasha kuwa na mawasiliano na wakili wake.

Emmanuel Mbasha aliyeambatana na ndugu zake wa kiume mahakamani hapo, anatuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 katika eneo la Tabata jijini Dar es salaam.
Previous Post Next Post