Unamkumbuka Yule Rapper kutoka Marekani laiyekata Uume wake, atoa sababu za kuukata uume wake

Unamkumbuka yule rapper kutoka Marekani  Andre Johnson ambaye alikata uume wake mwezi April na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja mjini Los Angeles, Marekani ameelezea sababu ya kuukata uume wake.


Rapper Andre Johnson

Johnson, aliishangaza jamii ya wanamuziki kufuatia kitendo chake cha kukata uume wake huko Kaskazini mwa Hollywood mwezi April. Madaktari walishindwa kuunganisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake na tangu hapo alikua kimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.

Wiki hii Andre aliamua kuelezea kwa nini alichukua uamuzi huo na kukiambia kituo cha televisheni cha E! nchini Marekani:”Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya, lakini nilikuwa najifahamu.”

Aliendelea,

“Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha maswaibu yangu. Suluhu yangu kwa maswaibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, mimi ni Mungu …..vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi. Mimi siko hapa ardhini si kwajili ya mwanadamu, bali Mungu.”

Matamshi ya Johnson yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya kiakili, lakini yeye anasisitiza kuwa yuko timamu na sio kichaa.

Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo.

“Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo, sikutaka kujiua,” alisema Johnson.

“Hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai na hilo ndilo jambo muhimu zaidi hata bila ya uume wangu. ”

Source:BBC
Previous Post Next Post