Kaa tayari kwa wimbo mpya kutoka kwa Ali Kiba 'Dar es salaam' anamzungumzia huyu msichana

Msanii aliyeht na wimbo kama Dushelele na zinginezo Ali Kiba, anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Dar Es Salaam’ ambao umetengenezwa katika studio za Combination Sounds chini ya producer, Man Walter.



Mdogo wake na Ali Kiba , Abdu, alisema kuwa wimbo wao wa pamoja ‘Pita Mbele’ unafanya vizuri na kinachofuata kwa sasa ni video na ujio wa wimbo mpya wa kaka yake.

“Tunashukuru Mungu wimbo unaenda poa sana, video bado kidogo ila kubwa zaidi ni ujio wa wimbo wa Ali Kiba ‘Dar Es Salaam, ni wimbo ambao unaelezea maisha fulani ya mtoto wa kike au msichana anayetumia madawa ya kulevya. Ni wimbo mzuri, producer ni Man Walter. Tunasubiri tu mwezi mtukufu umalizike ili mambo yafanyike,” alisema Abdu Kiba.
Previous Post Next Post