TIGO YAPOKEA TUZO YA UCHANGIAJI DAMU



Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Dr. Efesper Nkya akikabidhi cheti kwaMeneja wa Mpango wa Taifa wa Damu NBTS Dk. Efesper Nkya akimkabidhi cheti cha kushukuru mchango wa tigo kuchangia damu mkoa wa Lindi mwaka jana kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez kulia ni bi. Woinde Shisael Afisa wa  Ushirika wa Jamii wa Tigo.
                       
Tigo Tanzania  imekabidhiwa cheti cha shukrani kutoka kwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa msaada wake mkubwa wa kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kuchangia damu kupitia mpango wa kuchangia damu salama  ambao ulifanyika katika mkoa wa Lindi mwezi mwaka..
jana.
Mpango huu ulifanyikakatika mkoa wa Lindi Uwanja wa ILULU, na ulianza tarehe 25 Novemba 2012 na ulihitimishwa Desemba 1, 2012 kuashiria siku ya Ukimwi Duniani. Lengo kuu la zoezi hilo lilikuwa kuwaalika na kuhamasisha wachangiaji wa damu kwa njia ya hiari, pamoja na kutoa fursa kwa wanajumuia kupima VVU na kuelimishwa bure juu ya umuhimu wa tabia hatarishi za maambukizi ya VVU. Mpango huu ulikuwa na mafanikio makubwa kwani zaidi ya uniti 300 za damu zilikusanywa kutoka kwa wale ambao walishiriki. Maadhimisho ya mpango huo yaliongozwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika mkoa wa Lindi mwaka jana.
Mpango huo ulifanikiwa kuwaelimisha wanajamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu na jinsi zoezi rahisi kama hili linaweza kuokoa maisha ya mwanadamu, kwa kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, na mama wajawazito kwa kiwango cha asilimia 80% kati ya wapokeaji damu. “Sisi kama Mpango wa Taifa wa Damu Salama tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu kwa Tigo Tanzania kwa msaada wao mkubwa katika programu hii na imeonyesha kwamba wao wana moyo wa kuwasaidia Watanzania kuhakikisha wanaishi maisha bora na afya njema”, alisema Dk Efesper Nkya, Meneja wa Programu NBTS wakati akikabidhi cheti.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bwana Diego Gutierrez alisema akipokea cheti kuwa “kama Tigo tunajisikia heshima na fahari kubwa kuwa sehemu ya mpango huu wa kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa mchango wa damu salama, na tunafurahi kuwachangia Watanzania ili waishi maisha bora na afya njema. Ni furaha kubwa kwangu mimi kukubali hati ya shukrani kwa niaba ya Tigo Tanzania na napenda kuchukua fursa hii kushauri na kuwahamasisha Watanzania wote kuchangia damu salama, kwani mchango wao unaweza kuwa sababu kubwa katika kuokoa maisha ya mwanadamu mwingine
Previous Post Next Post