Dayna Nyange kufunga kwenye The Jump Off leo, uamuzi aliochukua baada ya kukosolewa kwenye nyimbo kuhusu kujichubua

Dayna Nyange ni mmoja kati ya wasichana wa kike ambao wamepata changamoto sana baada ya kutumia vipodozi vilivyobadili rangi yake ya awali (nyeusi) na kuwa nyeupe aka kujichubua.



Changamoto hiyo inatajwa pia katika verse ya Fid Q katika wimbo wa JCB ‘Cash za Kuzuga’ japo hakuna uthibitisho kama alizungumziwa yeye binafsi lakini mstari unamhusu.

Leo kwenye The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Dayna Nyange ambaye ndiye mkali wa The Jump Off atafunguka uamuzi aliouchukua baada ya kukutana na maoni yanayomshambulia kwa uamuzi wake huo kama msanii.

The Jump Off inakuwa hewani kupitia 100.5 Times Fm Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili usiku na Jabir Saleh aka Kuvichaka #KibongeToz, na DJ D-Ommy/DJ K-U.

Unaweza kusikiliza kwa njia ya mtandao kupitia tovuti hii, Bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.
Previous Post Next Post