Robin Thicke azidi kuchemsha, auza nakala54 tu za Albam yake Australia

Kama Robin Thicke angekuwa anaujua wimbo wa Snura Majanga, huenda ungekuwa wimbo wake wa muito wa simu. Lol!

Mwimbaji huyo ambaye ameachia albam aliyoipa jina la mkewe ‘Paula’ iliyobeba ujumbe maalum kumuomba radhi mkewe Paula Patton baada ya kuchepuka na kunaswa kisha akaachwa, amepata janga la aina yake baada ya albam hiyo kuendelea kufanya vibaya katika nchi mbalimbali ambapo nchini Australia imeuza nakala chini ya 54 katika wiki yake ya kwanza.




Kwa mujibu wa News.com.au, mwimbaji huyo mkubwa wa R&B ameshindwa hata kushika nafasi ya 500 katika chart ya Australia.

Hata hivyo, bado haijafahamika idadi kamili ya nakala hizo zilizotajwa kuwa chini ya 54 kwa kuwa mauzo ya nakala za albam ambazo ziko nje ya top 500 ya nchi hiyo huwa hayasajiliwi.

Paula imeshindwa kufanya vizuri pia katika nchi ya Uingereza ambapo imeuza nakala 530 tu, na Marekani imeuza nakala 24,000.

Ni kama watu wamechoka kusikiliza malalamiko yake kwa kuwa ameshaongea karibu katika kila jukwaa alilopanda kufanya show akimuomba msamaha mkewe Paula, na sasa ametoa albam nzima. Labda wengine wanataka aone madhara kamili ya uchepukaji.

Hii ni tofauti na albam yake ya mwaka jana ‘Blurred Lines’ ambayo ilishina nafasi ya kwanza Marekani na Uingereza ambapo Uingereza iliuza nakala 25,981 na Marekani nakala 177,000.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA