Mwanamuziki Mwana FA ambaye alishawahi kutamba na ngoma yake ya Bado nipo nipo kwanza na kuleta zogo mitaani baada ya kuwafanya vijana wengi kuutumia msemo huo,amefunguka na kusema kuwa atao hivi karibuni,
Mwana FA amefunguka hayo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa Eatv katika kipengele cha Kikaangoni Live,kinachokukutanisha na mtu maarufu au anayegusa jamii katika nyanja mbalimbali na kumpa nafasi ya kujibu maswali ya mashabiki wa ukurasa huo.
Mwana FA ameweka wazi kuwa siku za karibuni atafuta kauli yake ya kuwa Bado yupo yupo sana kama alivyoimba katika wimbo wake miaka kadhaa iliyopita,japo mkali huyo amedai ya kuwa atao ila itakuwa kimya kimya na watu watakuja kujua wakati tayari amekwisha weka jiko ndani.
mbali na kuoa Mwana FA ameelezea kazi yake mpya Mfalme ambayo kwa sasa inafanya vyema katika vituo mbalimbali vya Radio na kudai kuwa aliamua kumshirikisha G Nako na si Diamond Platnum kwa sababu yeye hafuati upepe katika kufanya kazi bali anafanya muziki mzuri ndiyo maana aliamua kumtafuta G Nako na kufanya naye kazi hiyo,ambayo amekili mpaka June atakuwa ameachia kichupa chake kwa mtaa.
SINA SABABU KUWASHIRIKISHA WASANII WAKUBWA WA NJE
Mwana FA ameweka wazi kuwa moja ya lengo lake kubwa katika muziki wake ni kuona anateka Tanzania na kufanya vizuri Tanzania kuliko nje ya Tanzania ndio maana amekuwa haoni sababu ya msingi kutaka kufanya kazi na wasanii wa nje licha ya nafasi ambayo huwa anapata.

Kwa kweli sioni sababu ya mimi kufanya kazi na wasanii wakubwa wa nje,sawa naweza kufanya nao kazi na je nikifanya nao kazi matokeo yake nini?na nafanya hivyo ili iweje? sasa si bora nifanye kazi na G Nako watanzania waielewe vizuri ili nitengeneze pesa ya kutosha,maana muziki mzuri ukifanya lazima utapendwa tu na hata kama utashirikiana na Jay Z lakini kazi ikiwa mbaya wataisikiliza tu na kuipotezea,so bora nifanye kazi nzuri ipendwe na kutengeneza pesa"
"Nilishakubaliana na Two Face wa Nigeria kufanya kazi lakini ndiyo hivyo tena nimekuwa mgumu kulifanyia kazi" aliongeza Mwana FA.
SIPO EAST COST
Mwana FA ambaye kipindi cha nyuma alishakuwa katika kikundi cha muziki wa Hip Hop ambacho kilikuwa maarufu sana kikiongozwa na King Crazy Gk amesema kuwa yeye pamoja na mwenzake AY hawapo katika Kundi hilo ili hali kundi hilo bado lipo na linaendelea na kazi yake ya muziki,Moja ya shabiki alitaka kujuwa na kujithibitishia juu ya tetesi zilizopo kuwa wanamuziki hao wamerudi kundi hilo la ECT.

MASHABIKI WANASEMA ANAKWEPA MASWALI
Baada ya kumaliza muda wake wa kuchat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV nilipitia Comments mbalimbali za watu huku nikiwa na jicho la kutafuta habari na kukutana na baadhi ya Comments ambazo zinamlalamikia mkali huyo kuwa anakwepa kujibu maswali yao na wengine wakionekana kutoridhika na majibu ya maswali yao.

Hamis Corleone Mwinjuma: mi nna redio mpka nizuie nyimbo zisipigwe aisee?
Mariam Ally :Sasa hapo umejibu ama umeuliza..? Mimi nakukubali sana wewe jamaa napenda kazi zako pia muonekano wako ni msaani ambae haupendi kujiweka ukatuni upo smart ila majibu yako F.
Mwembesi Zawadi Beatus: Huyu jamaa huu ukweli anaukwepa sijui kwanini?
Conzi Rhymez Maker :Mwembesi Hakuna mtanza anayeweza kudanganyika ss wengi tushaelimika