Msanii wa muziki wa nchini Kenya aliyeokoka, Size 8 ameweka wazi changamoto mbali mbali katika maisha haya mapya, kubwa zaidi ikiwa ni kupoteza mashavu mengi ya maonyesho, kunusurika ajali zaidi ya mbili na kuyumba kidogo kiuchumi.
Size 8 amesema kuwa, hata baada ya kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina Mateke, baadhi ya makundi katika imani hii mpya yalipinga kazi hii na kusema kuwa haijakaa kiinjili, na pia msanii huyu ameweka wazi kuwa kuna kipindi amekuwa akitokewa na watu wa ajabu usiku.
Hata hivyo, msanii huyu mkali wa muziki amesema kuwa, uamuzi wake wa kubadilisha aina ya maisha na kumgeukia Mungu ni kitu kizuri kabisa kuwahi kutokea katika maisha yake huku akisema kuwa maisha yake katika muziki wa dunia yalikuwa ni njia ya kifo.