Homa ya dengue yaanza kupungua

Serikali ya Tanzania imesema ugonjwa wa dengue umeonekana kuanza kupungua katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kutokana na wananchi kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa huo.

Msemaji wa wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, Nsachris Mwamwaja (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO hivi karibuni


Akizungumza na EATV, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja amesema mpaka siku ya jana wagonjwa wawili pekee waliokuwa wamelazwa na mmoja kuthibitika kuugua ugonjwa huo.
Aidha, Mwamwaja amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kusafisha mazingira ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Previous Post Next Post