Jokate aja na Biashara hii baada ya ile ya nywele na Ndala

Mwanamitindo Jokate Mwegelo ameibuka na ubunifu mpya wa sabuni ya kuogea inayokwenda kwa jina la Mo hiyo ikiwa ni baada ya kutesa na bidhaa ya ndala.



Jokate alisema uzinduzi wa sabuni hiyo unatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Juni 18, mwaka huu ambapo yeye na timu yake watatembea kwa miguu kutokea mjini (Posta) kuelekea Mbagala huku wakigawa zawadi kwa akina mama.



“Nashukuru nimeweza kubuni tena bidhaa nyingine, nataka kuwaambia wasichana wenzangu, wasilale. Tukitaka tunaweza kufanya makubwa. Nawashauri wapenzi wangu wakae barabarani kunisubiria nitapita na kundi langu la Kidoti ili niwapatie zawadi,” alisema Jokate.
Previous Post Next Post