Mexico yatoka sare tasa na Brazil, 0-0

Wenyeji  wa Kombe la Dunia 2014, Brazil wametoka suluhu na Mexico katika mechi yao ya pili ya kundi A. Brazil na Mexico wote kwa sasa wana pointi nne baada ya kucheza mechi mbili kila mmoja.

Mechi ya kwanza Brazil alimpiga Croatia mabao 3-1 wakati Mexico akimchapa Cameroon bao 1-0. Brazil anaongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao.

Warembo wa Brazil wakiishangilia timu yao.

Katika mechi hiyo, kipa wa Mexico, Guillermo Ochoa ameibuka nyota wa mchezo.

Kipa wa Mexico, Guillermo Ochoa akiokoa hatari langoni mwake.

Neymar akijaribu kuipangua ngome ya Mexico.


Soma Mashambulizi yalivyokuwa na dakika zake


90:00+02 Hii ni mara ya kwanza kwa Brazil kushindwa kuilaza Mexico katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia tangu 1978


90:00+01 Thiago Silva anamwangusha Aguilar90:00 +02 Mpira umekwishaBrazil 0-0 Mexico

90:00 Julio Cesar anaokoa mkwaju wa Mexico

88:56 KONA ya Mexico inapigwa nje na Guardado

85:57 Ochoa anaokoa Mexico kwa mara nyengine katika mechi hii anaupangua mpira uliokuwa unaelekea ndani ya neti

85:50 Neymar na Free kick nyengine

83 :40 Mexico Jimenez anachukua pahala pake Dos santos

82:00 Luiz Felipe Scolari anapanga kufanya mabadiliko baada ya safu yake ya ushambulizi kuwa butu mbele ya Mexico

81:03 Passi ya Neymar inakosa kumfikia Jo kwani Ochoa anatimuka na kuudaka

80:02 FREEKICK, ya Mexico inagonga ukuta na sasa Neymar anaongoza mashambulizi kuelekea Mexico

79:43 Thiago Silva anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumwangusha Hernandez

77:13 Hernandez anaangushwa na David Luiz

75 :12 Jo anapoteza nafasi nzuri akiwa amesalia na kipa pekee

73:10 Mexico inafanya Badiliko anaingia Hernandez anatoka Peralta

72:40 Brazil 53% Mexico 47

70:29 Mexico 0-0 Brazil

69:18 Achoa anaudaka mpira na kuupiga lakini Brazil wanauregesha kutekeleza shambulizi lingine.

68:20 Achoa anaokoa tena mkwaju wa Neymar na mpira unatoka nje na kuwa KONA.

67:27 Badiliko la Brazil .Anaondoka Fred na anaingia JO

66:12 Brazil inapoteza mpira na inakuwa ni goal Kick.

65:25 Thiago Silva anaangushwa na ni FREEKICK kuelekea lango la Mexico

62:49 Neymar anaipiga FREEKICK nje

61:39 FEEKICK kuelekea upande Mexico baada ya Vazquez kuoneshwa kadi ya njano

60:00 Mexico 0-0 Brazil.

58:20 Paul Aguilar aoneshwa kadi ya njano

55 :00 Dos santos anatuma kombora hafifu ambalo Julio Cesar anaukamata bila wasiwasi

54:00 Mexico wanatuma makombora kutoka nje ya eneo baada ya kushindwa kupenyeza ngome ya Brazil

52:00 KONA ya pili kwa Mexico .

51:50 Julio Cesar anatema nje mpira na inakuwa ni KONA

49:00 Neymar anapiga kona fupi ambayo inazuiliwa na Mexico


Brazil 0-0 Mexico

48:30 KONA kuelekea Mexico.

48:00 Rodriguez ainusru Mexico baada ya kumpiku Neymar na kupiga mpira nje .

45:30 Neymar anaangushwa na inakuwa ni Freekick kuelekea Mexico

45:00Kipindi cha pili kimeanza .

45 :00 +01 BRAZIL0-0 MEXICO



45 :00 +01 Refarii Cüneyt Çakir anapuliza kipenga na inakuwa mwisho wa kipindi cha kwanza .





Nyota wa Brazil

45 :00 +01 FREEKICK inapaa juu ya lango na mpira unatoka nje

45:00 FREEKICK kuelekea lango la Brazil

44 :10 Ramires anaoneshwa kadi ya kwanza ya manjano katika mechi hii kwa kumwangusha Aguilar

43:20 Ochoa anautema mkwaju wa Alves

42:45 FREEKICK kuelekea lango la Mexico

40:50 Aguilar afanya mashambulizi lakini sio ya kumbabaisha Julio Cesar

37:20 Mkwaju wa Julio Cesar unarejeshwa katika safu ya Brazil

35 45 Inachukuliwa kwa haraka lakini Dani Alves anamwangusha Layun na inakuwa ni freeKick

35 20 FREEKICK kuelekea Brazil;


Brazil 0-0 Mexico

34:40 KONA kueleka Mexico inazimwa na kipa Ochoa

32:30 Shambulizi la Brazil lazimwa na Aguilar na inakuwa ni Kona

31:30 Thiago Silva na Alves wanahimili mashambulizi ya Mexico

28 :50 Brazil yashambulia Mexico

27:55 Julio Cesar apangua mkwaju wa Mexico

24:50 Neymar aishambulia lango la mexico kwa mkwaju unaopanguliwa na kipa wa mexico Ochoa

24:30 Mexico inaendelea na mashambulizi katika lango la Brazil.

23:50 Mkwaju wa Herrera unapaa juu ya lango la Brazil





20:00 Brazil 0-0 Mexico

19: 00 Alves Brazil aonekana amemuangusha

17:15 Freekick kuelekea lango la Mexico

17:10 Neymar aangushwa tena na Rodriguez

13:50 Oscar anaangushwa na Paul Aguilar

12: 50 Mexico inaponea baada ya shambulizi lengine la Brazil katika lango lao

10'24 Shambulizi la Fred Brazil lazimwa kuwa ni Offside.

06:50 Freekick Kuelekea lango la Mexico,,,Mkwaju unagonga ukuta na kuondolewa



05'00 Shambulizi la Brazil linazimwa na safu ya ulinzi ya Mexico.




03'50 Mexico inaendelea kuidakua lango la Brazil

02'' Mpira unaondolewa na sasa ni wa kuruishwa kuel;ekea Brazil.

02'' Mexico inapata kona ya kwanza

21:54 Nyimbo za Taifa zinachezwa uwanjani sasa .

21:53 Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, David Luiz, Marcelo, Paulinho, Fred, Neymar, Oscar, Ramires, Luiz Gustavo

21:53 Mexico: Ochoa, Rodriguez, Marquez, Herrera, Layun, Dos Santos, Moreno, Guardado, Peralta, Aguilar, Vazquez

21:53Mexico iliilaza Cameroaon huku Brazil ikiibana Craotia katika mechi ya ufunguzi wa mashindano haya.


Brazil yailakika Mexico katika mechi ya pili ya kundi A



21:53 Brazil inachuana na Mexico katika mechi yao ya pili ya kundi A
Previous Post Next Post