Dullayo akiri kubadilisha style yake ya mwanzo kumemponza, apanga kurudi walikomzoea

Hitmaker wa Naumia Roho, Dulayo amekiri kuwa nyimbo zake kadhaa zimemwendea mrama ikiwemo ngoma ya ‘Watu Wabaya’ aliyofanyia katika Studio za Tongwe Records hali iliyomfanya kurejea kufanya style zake za awali.
Dulayo ameiambia Kikwetu Blog kuwa alianza kuhisi mapema kuwa ngoma yake haitopokelewa vizuri kutokana na kuimba kiutani. “Sikujipanga na sikuwa serious kihivyo nilikuwa na matatizo kidogo so nilikuwa nasikuisambaza katika media nyingi na wakati mwingine nilikuwa naulizwa kama nimeachia official lakini nilikuwa sina majibu. Lakini pia nimepata somo nataka kurejesha style zangu za zamani kama Naumia roho, Twende na Mimi au Mida ya Kazi,” alisema.




Dulayo amesema kudhihirisha kuwa style zake za awali ndizo zilizokuwa zikimfanya kuheshimika katika soko la muziki wa Bongo na nakukonga nyoyo za mashabiki, mwezi huu ataachia ngoma yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Mdebwedo aliyomshirikisha msanii kutoka kongo KENNEDO.
“Kwa sababu ya matarajio yangu kutofikia mafanikio, kwa hiyo hivi soon nitaachia Video pamoja na audio ikiwa katika miondoko ya Rap, nitaachia mwezi huu inafanana na miondoko ya Naumia Roho so fans wangu wakae mkao wa kumeza kwani watamsikia DULLAYO yuleyule wa kwao wakipindi cha nyuma”.

Kwa upande mwingine Dullayo akiwa kama baba mzazi wa mtoto wa kiume aitwaye, Sameer amesema mwanae huenda akaja kuwa mtu maarufu sana kutokana na dalili anazozionesha kupitia vitu anavyovipenda na anampa baraka zote za mafanikio.

“Mimi na mtoto mmoja anaitwa Sameer, ana umri wa mwaka mmoja, lakini bado sijaoa ila mtoto wangu namlea vizuri, mimi nafikiri mtoto wangu atakuwa star jinsi navyoona utundu wake nini licha ya kuwa anaumri mdogo lakini anapenda sana muziki, japo sipendi mwanangu aje kuwa mwanamuziki napenda asome awe msomi na elimu imkomboe na kuwa msaada mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla’.”
Previous Post Next Post