Young Killer azungumzia mahusiano, asema amefahamiana na mpenzi wake tangu akiwa darasa la 7

Young Killer Msodoki amesema alianza kufahamiana na mpenzi wake Halimaty tangu akiwa darasa la saba. Akiongea exclusively na Kikwetu Blog, Msodoki amesema Halimaty anatokea Mwanza pia.




“Mwisho wa siku ni demu wake ujue, yeye yupo, mimi nipo. Huwa nakaa naamini kwamba tayari yupo mtu ambaye ananijua kwasababu ananifahamu kabla hata sijawa staa,” amesema Msodoki.

“Kwahiyo siwezi kukaa kwa muda huu nikafocus kwamba natafuta niwe na demu wakati tayari nina mtu ambaye tayari kitambo toka hata sijawa supastaa, sijafanya chochote kile cha msingi halafu niwe na mwingine sasa hivi ambaye atakuja kunipenda tu kama Young Killer au Msodoki.”
Previous Post Next Post