Alshabab waua watu 10 kenya, ni baada ya kushambulia tena

Siku moja baada ya eneo la Mpeketu karibu na Lamu kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab na kuua watu takribani 50, kundi hilo limefanya shambulizi lingine katika eneo hio na kuua watu 10.



Polisi nchini Kenya wamesema kundi hilo limevamia kijiji kimoja usiku (June 16) na kufanya mashambulizi usiku kucha.

Kundi la Al Shabab lilidai kuhusika na shambulizi la kwanza na kueleza kuwa litaendelea na mashambulizi kama hayo nchini huko kwa lengo la kulipiza kisasi baada ya Kenya kupeleka wanajeshi wake Somalia kulisaka kundi hilo.
Previous Post Next Post