Chris Brown na Justin Bieber waingia studio, kurekodi wimbo kwa ajili ya Mashabiki

Justin Bieber na Chris Brown wameingia studio kupika muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wao Jumatatu, June 16.

Bieber amepost picha kwenye Instagram akiwa na Chris Brown na kuandika , “Studio, me and CB did 1 for the fans.”



Bado halijafahamika jina la wimbo na lini wimbo huo utatoka na utakuwa kwenye albam au ni wimbo utakaokuwa unajitegemea.

Hata hivyo, sio mara ya kwanza kwao kufanya wimbo pamoja, mwaka 2011 Chris Brown alimshirikisha JB kwenye ‘Next to You’ uliokuwa kwenye albam yake ya F.A.M.E.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa