Video: Mwanamuziki apasuliwa kooni huku akiimba

Tukio la upasuaji la aina yake limeripotiwa nchini Ufaransa ambapo mwimbaji Alama Kante ambaye ni raia wa Guinea anayeishi nchini humo amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba.

Madaktari waliofanya upasuaji huo wamesema waliamua kuchukua hatua hiyo ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.




Imeelezwa kuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji mwimbaji huyo alipewa dawa za kumfanya asihisi maumivu yoyote.

Alama Kante alikuwa na hofu kubwa kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini madaktari wake ndio waliopendekeza kuwa aimbe huku akiendelea kufanyiwa upasuaji hatua ambayo haijawahi kuchukuliwa duniani.

Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya Henri Mondor na uliongozwa na Profesa Giles Dhonneur ambaye amesema anatumaini mambo yatakuwa sawa.



Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao.

Previous Post Next Post

Popular Items