Video: Pharrell atoa video mpya ya ‘Marilyn Monroe’.

Hit maker wa 'Happy' Pharrell Williams ametoa video ya single yake mpya ‘Marilyn Monroe’ jana, pamoja na video hiyo pia ameshare cover rasmi ya single hiyo ambayo inaongea kitu kuhusiana na lawama alizopokea alipotoa cover ya album yake mwanzoni mwa mwaka huu.



Mwanzoni mwa mwaka huu hit maker wa ‘Happy’ alipata lawama za mashabiki wake baada ya kutoa cover ya album ‘G I R L’ iliyokuwa na picha ya wasichana watatu pamoja na yeye, wakimlaumu kwa kutoweka msichana wa Kiafrika katika cover hiyo.

Jana Pharrell ametoa cover ya single yake mpya ‘Marilyn Monroe’ ambayo ina picha ya msichana wa Kiafrika ikiashiria kuwa anajaribu kuwaridhisha mashabiki ambao walimkosoa mwanzo.

Hivi karibuni Pharrell alimwambia Oprah jinsi alivyojisikia vibaya kwa kukosolewa kutoweka msichana mweusi licha ya kuwa mmoja kati ya wasichana wale ana asili ya Afrika-Amerika japo baba yake ndio mweusi huku mama yake akiwa ni mzungu hivyo kusababisha awe mweupe kwa rangi.

Tazama video ya ‘Marilyn Monroe’ iliyotoka tarehe 23



Previous Post Next Post

Popular Items