Wema kuifufua Endless Fame upya baada ya ukimya wa muda

Muigizaji mwenye vituko vingi katika filamu nchini Wema Sepetu ‘Wema’, anatarajia kuifufua upya kampuni na lebo iliyokuwa ikisimamia kazi za wanamuziki ‘Endless Fame’.


Habari zinapasha kuwa mwanadada huyo baada ya kimya cha muda mrefu Wema ameamua kurudisha tena kampuni hiyo kwa lengo la kujijenga zaidi kisanaa na pia kuongeza wigo wa filamu nchini.

Chanzo hicho kilisema katika kuhakikisha lebo hiyo inarudi upya, msanii huyo aliamua kusafiri kuelekea China pamoja akiwa na meneja wake Martin Kadinda na meneja wa wasanii ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kampuni hiyo Petman Wakuache.
Previous Post Next Post