Video: Msichana aliyepigwa na Chidi Benz alijeruhiwa vibaya usoni na kichwani, mtazame hapa

Msanii wa Miondoko ya Hip Hop Chidi Benz alimjeruhi vibaya msichana anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa zamani, Mwanaisha Kiboye. Kwa mujibu wa maelezo aliyoipa Global TV, Mwanaisha anasema alimkuta Chidi Benz maeneo ya Buguruni akiwa na mpenzi wake na kumsalimia hali iliyomchukiza rapper huyo aliyebinua meza waliyokuwa wamekaa na kuanza kumpiga.


Hata hivyo Chidi Benz aliyekamatwa, kupanda kizambani kwenye mahakama ya Ilala kwa kosa la kujeruhi na kukutwa na bangi, ametoka nje kwa dhamana ya shilingi laki moja, kitendo ambacho kimewasikitisha ndugu wa Mwanaisha wanaosema alimjeruhi mno kiasi cha kukaribia kumuua.



“Ukiangalia mgonjwa mwenyewe baada ya muda anapoteza fahamu, anaweza akapoteza fahamu nusu saa. Kwahiyo hapa tunafanya process za kufanya CT-Scan ya kichwa na ambayo gharama yake ni laki 3 kwa private na laki mbili kwa serikali,” alisema Oliver ambaye ni rafiki wa Mwanaisha,.

Previous Post Next Post