Oscar Pistorius ajitetea dhidi ya kesi ya kumuua mpenzi wake, adai huona mauzauza na akiamka husikia harufu ya damu

Mwanariadha Oscar Pistorious amepanda kizimbani leo (April 7) kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya kuumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya Valentine mwaka jana.

Mama mzazi wa Reeva Steenkamp, anaefahamika kwa jina la June yuko mahakamani akisikiliza kesi hiyo.


Akiongea kwa unyonge, Ocar Pistorious ameanza kwa kuiomba radhi familia ya Reeva na kueleza kuwa anafahamu maumivu wanayoyapata lakini angependa wafahamu kuwa alikuwa anajaribu kumlinda Reeva.

Pistorious mwenye umri wa miaka 27, ameeleza kuwa hivi sasa anashambuliwa na tatizo la kusaikolojia na anaona mauzauza usiku kiasi kwamba hawezi kulala kutokana na tukio hilo na kwamba hata anapoamka husikia harufu ya damu.

Ameongeza kuwa kutokana na tukio hilo, hataki tena kumiliki silaha ya moto na kwamba ana walinzi mlangoni kwake hasa nyakati za usiku.

Pistorius anaeleza kuwa alipiga risasi akidhani ana mpiga jambazi aliyevamia nyumbani kwake na kumbe alikuwa anampiga mpenzi wake.

Hivi sasa wameingia katika muda wa mapumziko ili akapate chakula cha mchana na kesi itaendelea baadae.
Previous Post Next Post

Popular Items