Ikulu ya Marekani inaweza kuzuia watu maarufu kujipiga picha na Obama 'Selfie'

Ikulu ya Marekani inaweza kuzuia tabia ya watu maarufu wanaokutana na Obama kujipiga picha wakiwa nae (‘Selfie’) kwa kuwa picha hizo zinaweza kutumika vibaya kama sehemu ya matangazo.

Katazo hilo linakuja baada ya kampuni ya simu ya Sumsang kuitumia picha ya mchezaji maarufu wa Marekani David Ortiz aliyopiga na Obama kwa kutumia simu yake baada ya kumtembelea ikulu.




“Tumefurahi sana kuona picha maalum, ya tukio la kihistoria David Ortiz aliyopiga na Galaxy Note 3 wakati ameitembelea White House.” Sumsang iliiambia Boston Globe.

Kwa mujibu wa AFP, mshauri mkuu wa rais Barack Obama, Dan Pfeiffer ameeleza kuwa Ikulu ya Marekani inaweza kuzuia upigaji picha wa aina hiyo.

“Mtu anaetumia mfanano wa rais kutangaza bidhaa…hilo ni tatizo. Labda hii itakuwa mwisho wa ‘selfies’ zote.” Alisema Dan Pfeiffer.

Baada ya picha hiyo kuwekwa kwenye akaunti ya twitter ya David Ortiz ilikuwa retweeted zaidi ya mara 45, 000 na kupata zaidi ya favorites 48,000.
Previous Post Next Post