Video: Wasichana wanne wa Tanzania wamekamatwa Macau China wakijiuza

Wasichana wanne wa Tanzania wanadaiwa kukamatwa huko Macau, China baada ya kujihusisha na biashara ya ngono, ambapo ni kinyume na sheria za China.



Blogger anayeishi nchini Uingereza, Jestina George ameandika:

Baada ya kuweka audio clips za hao mabiniti wakilalamika na kuomba msaada ndipo nilipo amua kuanzisha campaign ili kuwasaidia mabinti hao walioko MACAU. Nilijaribu kwa hali na mali kutafuta mawasilano ili kujua wako wapi na kama habari hizi ni za ukweli. Nilibahatika kuongea na baadi ya watu wanao ishi huko na wakanihakikishia kwamba habari hizo ni za kweli na walinihakikisha kwamba kuna mabinti wadogo sana wanaotumiwa katika biashara hiyo haramu na wanahitaji msaada haraka iwezekanavyo ingawa wanaogopa kutokana na vitisho wanavyopewa na hao wanaojiita mabosslady au mama zao.




Baada ya hapo ndipo harakati za kuwasaidia zilipo anza na kwa kushirikaina na kaka yangu KWAME tukawasiliana na shirkia la IOM (International Organization for Migration) ambao ndo mara nyingi husaidia watu wenye matatizo kama haya kurudi nyumbani wakatushauri cha kufanya so tukawasiliana na police wa MACAU na kuwaelezea tatizo zima na ndipo jana Jumamosi 5 April 2014 walifanikisha zoezi hilo kama inavvyo repotiwa hapa chini kwenye taarifa ya habari ya TDM ENGLISH NEWS ya MACAU.
Previous Post Next Post

Popular Items