Video: Mustapha na Nyota Ndogo wakutanishwa na NTV, ni sakata la picha alizopiga na Huddah

Kituo cha runinga cha NTV cha Kenya kimefanya zoezi la kukata mzizi wa kutoelewana kati ya ColonelMustapha na Nyota Ndogo aliyeongoza maandamano ya kupinga vikali picha za Colonel Mustapha na Huddah Monroe kwa madai kuwa zinadhalilisha wanawake.

Katika mahojiano hayo, kabla hajaunganishwa kwa njia ya simu na Nyota Ndogo, Mustapha alipewa nafasi ya kueleza kilichotokea kati yake na Huddah Monroe ambapo aliendelea kusisitiza kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Huddah na wakakosana baadae.


“Kilichofanyika…si watu walikuwa in love wakakosana...that’s it.” Alisema Mustapha.

Kauli hii inaweza kuendelea kuwa mwiba kwa Huddah ambaye anadai hajawahi kuwa na uhusiano na Mustapha na kwamba yote yaliyofanyika ilikuwa ni drama ya kupangwa na alilipwa pesa kupiga picha ili kumpa ‘kick’ Mustapha.

Akieleza kuhusu majibishano makali yaliyoendelea kwenye mitandao ya kijamii kati yake na Huddah, Mustapha alidai mashabiki wao ndio wamekuwa wakigombana.

“The issue is fans wangu na fans wake wamekuwa wanafight kwa social media. Kwa sababu kuna time alikuwa anasema mimi low class. So pia kuna mafans walikuwa wanasema kuwa kama mimi ni low class kwa nini hivyo vitu vyote vilifanyika, there is pictures, we went to news na akasema tuko pamoja na akinipata na demu atanishoot. So fans walikuwa wana-wonder nini inaendelea…





Mustapha aliingia kwenye kile ambacho kiliwaudhi wanawake wa Pwani ambapo nae alikuwa ana yake ya kuwaambia wanawake hao walioandamana kuwa aliyepiga hizo picha ni mtu mzima na alifanya kwa matakwa yake.

Kauli hiyo ilimuudhi Nyota Ndogo alipoirudia wakati wameunganishwa, “ yeye kama mtu mzima kwa nini alikubali kupiga nao picha?” Nyota Ndogo aliuliza.

Nyota ndogo alimbana Mustapha na kuyaita majibu yake ni ya kitoto kuonesha jinsi ambavyo hakutumia akili kiutu uzima kudeal na hilo tatizo.
“Unaona sasa utoto niliokuwa nauita? Mimi namwambia yeye, yeye anamrushia mtu mwingine, unaona mpaka majibu yake ni ya kitoto.”

Hata hivyo, Mustapha alikuwa mpole na kuomba radhi kwa mara nyingine kwa kile kilichotokea na walichokuwa wakimkosoa kuwa amedhalilisha wanawake kwa ujumla.
Previous Post Next Post